Monday 30 December 2013

Joh na Nikki wa pili kufanya video tatu january 2014


Ndugu wawili kutoka kundi la Weusi nchini Joh Makini na Nikki wa Pili wanatarajia kuachia video tatu kwa mpigo ndani ya mwezi january 2014 kwa nyimbo zilizokosa video mpaka sasa.Rapper joh makini alisema video ya kwanza wanatarajia kufanyia Arusha chini ya director Nisher wiki hi na wanatarajia kuondoka 31 (kesho) pamoja na G Nako
Pia alisema video ya pili ambayo itakua single ya "Bei ya mkaa' wanatarajia kuifanyia jiji Dar es salaamu chini ya director Adamu Juma katika wiki ya pili ya mwezi wa kwanza.
Joh makini aliongeza kwa kusema video yake ya tatu ni ile aliyofanya na Fundi samwel "Nikumbatie'ambayo video hiyo anatarajia kufanya na director ya nje 
“Sijajua nafanya na nani video ya Nikumbatie lakini nataka kufanya na director wa nje…naweza kuja au mimi kwenda ila nitajua nikishaamua ni nani nafanya nae” alisema joh 

No comments:

Post a Comment