Thursday 19 December 2013

KIDOTI CLUB YAFANYIWA UZINDUZI

 
   Mbunifu wa  mavazi na Mjasiriamali nchini, Jokate Mwegelo  jana amefanya uzinduzi wa club yake itanayoitwa ‘Kidoti Club’.“Ni huduma za SMS, watu wanajiunga kwenye ‘Kidoti Club’ na watakuwa watapata tips mbalimbali za urembo, mitindo na mambo ya lifestyle, inspiration… na baadae kutakuwa na zawadi za kushindaniwa,
     Kuhusu maboresho ya nywele Joketi alisema "Tulipotoa bidhaa za mwanzo, honestly kuna watu walisema kuna vitu ambavyo walipenda viboreshwe zaidi na sasa hivi kweli vimeboreshwa. Packaging imeboreshwa, sasa hivi tumeweka kifungo.” "Ni bidhaa ya nyumbani, ni bidhaa inayotengenezwa na mwanamke, kwa hiyo naelewa wanawake wanahitaji nini. Ni bidhaa ambayo bei yake sio kubwa lakini quality yake ni nzuri, mtu anaweza kuvaa kwa mwezi na isimuwashe kichwani. Kwa hiyo ni kitu ambacho tumekipackage vizuri, vilevile kina muonekano mzuri, rangi tumechagua nzuri. Kwa hiyo zinashindana vizuri tu na bidhaa za nchi nyingine,” ameongeza.
     Joketi alimaliza kwa kusema "“Nimelenga hasa East na Central Africa, kwa sababu nimeshaanza kupata order kutoka Burundi, Kenya..yeah kwa hiyo ni East na Central Africa. Kuhusu mikoani, sasa hivi mimi nadeal kwanza na Agents, agents wangu wengi wako Kariakoo na ndio wanaopeleka mikoani. Sijaanza kupeleka moja kwa moja mikoani, hiyo ndio njia ninayoitumia kupeleka mikoani.”

No comments:

Post a Comment