Monday 23 December 2013

Huu ni ushauri kwa Rappers wa Tanzania toka Mweledi wa hiphop California kutumia zaidi ya lugha ya kiswahili

Wasanii wanaofanya muziki wa hip hop Tanzania wameshauriwa kutumia zaidi lugha ya Kiswahili katika muziki wao ili kujitangaza zaidi duniani kwa lugha ya kwao kuliko kuiga lugha ya kiingereza.
Ushauri huo umetolewa na mfuatiliaji au mweledi wa masuala ya hip hop anayejihusisha na utengenezaji wa makala zinazohusu hip hop toka miaka ya 1990, Jacob ‘Kahlil’ Fantauzzi toka California, Marekani.
Kahlil amefunguka kupitia katika kituo kimoja cha radio jiji Dar wakati akipiga story na mtangazaji wa kituo hicho, ambapo amesema kuwa ni vizuri pia wasanii wakaongeza na vionjo vya nyumbani ili kuupa muziki wao ladha ya kipekee tofauti na ile ya Marekani.
“Nadhani wakati hip hop ilipoanza katika sehemu mbalimbali za dunia, muda mwingi watu walianza kama kuiga hata mashairi na kuyaweka kwenye lugha zao na kusema ‘ooh sasa tunarap’. Lakini sasa inaonesha maendeleo ya wachenguaji, na inaonesha maendeleo katika utamaduni wa hip hop, pale ambapo wazawa wanaweza kutumia lugha zao wenyewe, mtindo wao wenyewe na vionjo vyao vya muziki. Ameeleza Kahlil.
Ametolea mfano wa makundi ya hip hop kutoka Cuba na Hispania waliong’ang’ania kutumia lugha zao na kuachana na kuiga kiingereza, na mwisho wa siku wakajikuta wanashika sehemu kubwa ya dunia na kupata tuzo za kimataifa.
Kahlil amekuwa anafanya makala na filamu zinazohusu hip hop, na amekuwa wakizunguka nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kufanya makala na filamu hizo ambazo zinapatika kupitia tovuti ya fistup.tv

No comments:

Post a Comment